Dodoma FM

Jamii imetakiwa kusoma na kuielewa mikataba mbalimbali kabla ya kusaini

3 November 2021, 1:40 pm

Na; Shani Nicolous.

Wito umetolewa kwa jamii kusoma na kuelewa mikataba mbalimbali wanayopewa katika makubaliano kabla ya kuisaini.

Wito huo umetolewa na msaidizi wa kisheria kutoka kata ya Dodoma Makulu Bw. Kapesa Youngson wakati akizungumza na Taswira ya habari na kusema kuwa wananchi wengi wanakutana na changamoto mbalimbali ya mikataba kwakuwa wanaisaini bila kusoma na kuielewa.

Amesema kuwa ni vyema kabla ya kuisaini ni vyema kushirikisha baadhi ya watu ili kushauriana na kuepuka matatizo na maumivu yatakayojitokeza baadaye.

Amesema kuwa ili mkataba uweze kuwa halali ni lazima ufuatae taratibu za kisheria na mashahidi huku ikifuatiwa na utashi wa wahusika katika makubaliano hayo .

Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema kuwa mikataba mingi imekuwa ikiwaumiza watu kwakuwa wengi wao husaini kwa shida zao bila kuielewa ,hivyo wameiomba serikali kuweka na kusimamia kwa ukaribu sheria za mikataba mbalimbali nchi.

Jamii bado ina kiu ya elimu zaidi juu ya mikataba na hasa umakini wa kusoma vizuri na kuilewa kabla ya kusaini.