Dodoma FM

Michese waishukuru serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa shule

16 October 2023, 7:03 pm

Picha ni wakazi wa Michese wakisafisha eneo hilo itakapo jengwa shule hiyo .Picha na Thadei Tesha

Kwa mujibu wa viongozi wa mitaa hiyo wanasema kuwa fedha kiasi cha shilingi milioni mia tano zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi huo.

Na Khadija Ayoub.

Baadhi ya wananchi katika eneo la michese jijini Dodoma wameishukuru serikali kwa kuwapatia kiasi cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Michese.

Kufuatia kutolewa kwa fedha hizo baadhi ya wananchi wamejtokeza kwa ajili ya kufanya usafi katika eneo hilo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi huu.

Dodoma Fm imefika katika eneo hilo na kukuta shughuli za usafi zikiendelea na hawa ni baadhi ya wananchi katika eneo hili hapa wanaeleza namna shule hiyo itakavyosaidia kuondoa changamoto za wanafunzi kutembea umbali mrefu.

Sauti za wananchi.
Wakazi wa Michese wakifanya usafi katika eneo hilo .Picha na Thadei Tesha.

Baadhi ya viongozi  wanaozunguka eneo la mradi huo ikiwemo bw sostenes Abeli mwenyekiti  mtaa wa bwawani na Bw. Godfrey wa mtaa wa nzinje wamesema mradi huo utakwenda kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabili na wameahidi kuendelea kushirikiana na wananchi katika ujenzi.

Sauti za viongozi.