Dodoma FM

Watumiaji wa nishati watakiwa kuwa na nidhamu ya matumizi

29 May 2026, 17:52

Picha ni Spiradson Kagaba afisa viwango TBS .Picha na mtandao.

Ni vizuri kubadili tabia ya matumizi yasiyofaa ya umeme kutokana na umeme mwingi kupotea bila sababu.

Na Jerome John.

Watumiaji wa nishati ya umeme nchini wametakiwa kubadili tabia ya utumiaji wa nishati holela kwa kupunguza matumizi ya nishati hiyo.

Wito huo umetolewa na Joyce Msangi afisa mwandamizi kutoka wizara ya nishati katika mdahalo wa matumizi bora ya nishati uliowashirikisha wadau mbali mbali kuhusu sera za matumizi bora ya nishati.

Msangi amesema kuwa ni vizuri kubadili tabia ya matumizi yasiyofaa ya umeme kutokana na umeme mwingi kupotea bila sababu wakati umeme huo ungetumika katika matumizi mengine ambayo yangesaidia kiuchumi,viwandani,majumbani na sehemu nyingine.

Aidha amebainisha kuwa kumekuwepo na tabia za baadhi ya watu kuacha vifaa vinavyotumia umeme vikiwa vimewaka bila kuzima na huo ni upotevu wa umeme badala yake ameshauri kutumia vifaa vinavyotumia nishati ndogo bila kuongeza gharama kubwa.

Sauti ya Joyce Msangi .

Kwa upande wake Spiradson Kagaba afisa viwango Tbs amesema kuwa elimu ya umuhimu wa kutumia vifaa bora ni muhimu katika jamii na kuhakikisha jamii hiyo inatumia bidhaa ambazo zimekidhi viwango vya ubora kuepukana na madhara yanayoweza kutokea.

Vile vile ameshauri kutumia wataalamu wenye weledi katika maeneo ya ujenzi au kufunga nyaya za umeme katika nyumba ili kuondokana na majanga ya ajali za moto yanayoweza kusababishwa na watu wasio kuwa na weledi yaani vishoka.

Sauti ya Spiradson Kagaba.