Dodoma FM

Mwananchi Mpendo anusuru vitongoji vitatu adha ya maji

1 August 2023, 4:17 pm

Wananchi wa eneo hilo wamemshukuru Leonard kwa kuwaokoa na changamoto hiyo ya maji. Picha na Mulika Dodoma Tv.

Waswahili wanasema penye nia pana njia hivyo ndivyo Leonard Daudi amesaidia kutatua changamoto kubwa ya maji katika eneo lake.

Na Mindi Joseph.

Mwananchi mmoja katika kijiji cha Hamia kata ya Mpendo wilayani Chemba mkoani Dodoma amejitolea kuchimba kisima cha maji  na kunusuru vitongoji vitatu na changamoto ya maji.

Leonard Daudi ni mfugaji na mkazi wa eneo hilo anasema kilichomsukuma kuchimba kisima cha maji ni kutokana na  kero ya maji kwa kipindi kirefu sasa.

Kisima hicho kimewapa ahueni wananchi wa eneo hilo.

Sauti ya bwana Leonard Daudi.
Picha ni mkazi wa kijiji cha Mpendo bwana Leonard Daudi aliyejitolea kuchimba kisima cha maji. Picha na Mulika ya Dodoma Tv.

Wananchi wa eneo hilo wamemshukuru Leonard kwa kuwaokoa na changamoto ya maji.

Sauti za wakazi wa Mpendo.

Diwani wa kata ya Mpendo wilaya ya Chemba Bw. Benard Kapaya Naye alikuwa na haya ya kusema.

Sauti ya diwani wa kata ya Mpendo