Dodoma FM

Dodoma: Wafanyabiashara kituo cha Mnada Mpya waomba kuboreshewa mazingira

24 May 2023, 7:49 pm

Mwonekano wa vibanda vya wafanyabiashara katika eneo hilo la Mnada Mpya.P icha na Thadei Tesha.

Pamoja na sababu hizo wafayabiahara hao wanasema kuwa ni vyema serikali kuendelea kuboresha mazingira ikiwa ni pamoja na kuruhusu mabasi kuingia ndani ya kituo hicho ili waweze kupata wateja.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya wafanyabiashara katika kituo cha mabasi cha Mnada Mpya jijini Dodoma wameiomba serikali kuboresha mazingira ya kituo hicho ili kutoa hamasa kwa wananchi kufanya biashara katika eneo la soko lililo karibu na kituo hicho.

Dodoma Tv imefika na kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara katika kituo hicho ambapo pia lipo soko ingawa halina wafanyabiashara hapa wanasema kuwa miongoni mwa sababu zinazopelekea kutokuwepo katika eneo hilo ni pamoja na ubovu wa miundombinu ya kituo.

Sauti za wafanyabiashara .
Muonekano wa vibanda vya wafanyabiashara katika eneo hilo la Mnada Mpya.Picha na Thadei Tesha.

Aidha wameongeza kuwa awali walikuwa wakifanyia biashara katika soko hilo bada ya serikali kuwahamishia kutoka eneo la mbele ya kituo cha mabasi lakini kutokna na ukosefu wa wateja imewalazimu kurudi katika eneo la mbele la kituo hicho.

Sauti za Wafanyabiashara.