Dodoma FM

Kigoma Ujiji kupima, kusajili makazi 10,000 katika mitaa 25

4 September 2023, 4:09 pm

Picha ni wadau wakiwa katika mkutano huo kujadili upimaji ardhi mapema leo. Picha na Wizara ya Ardhi.

Mradi huu umelenga kuboresha usalama wa milki za ardhi kwa kupanga, kupima na kusajili milki za ardhi zipatazo milioni 2.5 zinazojumuisha hatimilki 1,000,000 na Leseni za Makazi 1,000,000 katika maeneo ya mijini na Hati za Hakimilki za Kimila 500,000 vijijini.

Na Seleman Kodima.

Manispaa ya Kigoma Ujiji  inakusudia kupanga, kupima na kusajili makazi 10,000 katika mitaa 25 kupitia mradi wa uboreshaji wa Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP)

Pia mradi huo  umelenga kusimika mfumo unganishi wa kielektroniki wa kuhifadhi kumbukumbu za ardhi (ILMIS) katika ofisi zote za ardhi za mikoa na halmashauri mbalimbali.  

Manispaa ya Kigoma Ujiji ni miongoni mwa halmashauri 34 nchini zinazotekeleza mradi wa Kuboresha Usalama wa Milki za Ardhi mijini.

Aidha katika Manispaa hiyo, utekelezaji wa mradi huu ulianza  mwezi Juni, 2023 ikiwa na lengo la kutambua, kupanga, kupima na kusajili milki zipatazo 10,000 ambazo zitamilikishwa kwa wananchi wa Manispaa ya Kigoma.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Kigoma Salum Kalili wakati akizungumza na wadau leo wakati wakijadili utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa usalama wa milki za ardhi wilaya ya Kigoma Ujiji ambapo amesema  kuwa ardhi iliyopimwa wilayani Kigoma Ujiji  itaongezeka thamani pindi wananchi wa eneo hilo watakaposhiriki katika utekelezaji wa mradi wa  huo.

Sauti ya Mh. Salum Kalli.

Aidha amesema kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM imetoa mwongozo wa namna ya kuboresha miji inayokua ,upangaji wa miji mbalimbali ndani ya Tanzania pamoja na urasimishaji wa maeneo mbalimbali.

Sauti ya Mh Salum Kalli

Akizungumza katika Mkutano huo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Evance Mdee  amewahakikisha timu za watalaamu kuwapa ushirikiano katika kuboresha na kutekeleza mradi huu .

Amesema kuwa Hadi sasa zaidi ya makazi 4,000 yametambuliwa katika Kata ya Kibirizi, michoro ya viwanja 1,500 imeandaliwa na wananchi wa Mtaa wa Kibirizi wanaendelea kuhakiki taarifa zao za umiliki na kazi inaendelea.