Dodoma FM

Wafanyabishara sabasaba wafurahia mazingira ya soko

24 January 2024, 10:17 pm

Picha ni muonekano wa soko la sabasaba msimu huu wa mvua ambapo awali palikuwa panajaa tope mvua inaponyesha. Picha na Thadei Tesha.

Soko la Sabasaba ni miongoni mwa masoko makubwa yaliyopo Jijini Dodoma ambayo ni maarufu kwa uuzwaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo mbogamboga matunda na mavazi.

Na Thadei Tesha.
Wafanyabiahara wa soko la sabasaba Jijini Dodoma Wameelezea kufurahishwa na hali ya mazingira ya sasa sokoni hapo ukilinganisha na kipindi cha nyuma wakati wa msimu wa masika.

Hili ni soko la Sabasaba soko la sabasaba lililopo Jijini Dodoma Soko hili limejizolea umaarufu kwa kuuza bidhaa mbalimbali ikiwemo bidhaa za mbogamboga matunda.

Picha ni Muonekano wa ardhi ya eneo hilo baada ya ukarabati . Picha na Thadei Tesha.

Kwa muda mrefu soko hili lilikuwa na changamoto ya njia za kuingia ndani ya soko hususani katika msimu wa masika jambo ambalo lilikuwa likiwapa changamoto hususani katika sula la kukosa wateja lakini kwa sasa hali ni tofauti kufuatia marekebisho yaliyofanyika kwa sasa Wafnyabiashara katika soko hili wanasema kuwa kwa sasa hali ni shwari.

Sauti za wafanyabishara .

Dodoma Tv imefanya mahojiano na mwenyekiti wa kamati ya miundombinu soko la Sabsaba ambapo anasema kuwa ushirikiano wa viongozi pamoja na wafanyabiashara hao ndio uliochangia maboresho ya soko hilo.

Sauti ya mwenyekiti wa kamati ya miundombinu soko la Sabsaba.