Dodoma FM

Wakazi wa Nzasa waiomba serikali iwasaidie kukamilisha ujenzi wa shule

27 January 2022, 2:45 pm

Na ;Victor Chigwada.

Wanafunzi wa kijiji cha Nzasa Kata ya Chiboli hulazimika kutembea kila siku  Zaidi ya kilomita 15 kuifata shule ilipo.

Wakizungumza na Dodoma Fm baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa umbali mrefu umekuwa changamoto kwa wanafunzi wa umri mdogo wanaolazimika kutembea kwa muda mrefu kufika shuleni

Imeelezwa licha ya  umbali huo kwa wanafunzi lakini bado wanakumbana na msitu mkubwa pamoja na  korongo ambavyo vyote ni hatari kwao.

Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Wiliamu Chewu ameeleza katika kukabiliana na changamoto hiyo wananchi walijitolea kujenga madarasa manne na ofisi ya walimu lakini wamekwama fedha za kupaua

Bw.Chewu ameiomba Serikali kuwasaidia kupaua madarasa hayo ili kupunguza umbali wanaotembea wanafunzi  pamoja na kuwaepusha na hatari ya kuvuka msitu na korongo

Mazingira hatarishi yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa kuwakatisha tamaa wanafunzi kwa kuhofia usalama wao pamoja na kuchoka kutembea umbali mrefu