Dodoma FM

Gesi ya ukaa hatari kwa mazingira

25 April 2024, 6:38 pm

Wastani wa kiwango cha joto duniani kwa sasa ni nyuzijoto 1.1°C zaidi ikilinganishwa na mwanzoni mwa karne iliyopita.Picha na Mariam Kasawa.

Kuboresha na kutunza mazingira ardhini na baharini ni mojawapo ya mikakati mikuu ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Na Mariam Kasawa.
Inaelezwa kuwa uzalishaji wa gesi ya ukaa usipopunguzwa kwa asilimia 7.6 kila mwaka dunia haitaweza kufikia nyuzijoto 1.5 za kiwango cha joto zinazolengwa kufikiwa chini ya Mkataba wa Paris.

Iwapo kiwango cha joto kitaendelea hivyo bila kudhibitiwa, itakuwa na madhara mabaya zaidi kwa binadamu, ekolojia na katika uchumi, na kusababisha uhaba wa chakula, mioto mikuu, kuongeza urari wa bahari na kusababisha hali mbaya zaidi ya hewa.

Wanafunzi kutoka Chuo cha Veta Dodoma wao wanasema endapo kutawekwa usimamizi na sheria kali itasaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Misitu, maeneo oevu, na mifumo mingine ya ekolojia ni muhimu katika kukabiliana na hali mbaya ya hewa, kutunza makazi, mimea, usambazaji wa maji na miundo ni muhimu katika kutunza na kuhifadhi mazingira kama anavyo tueleza Afisa mazingira kitengo cha udhibiti wa taka ngumu Jijini Dodoma.

Picha ni Mwanafunzi chuo cha VETA jijini Dodoma akiongea na Dodoma Tv. Picha na Mariam Kasawa.

Tanzania ipo kwenye mpango wa kupunguza hewa ya ukaa kwa asilimia 20% ifikapo mwaka 2030 hayo aliyasema Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza alipokuwa Mkoani Ruvuma march 16 2024,

Ripoti ya UNEP ya 2020 Emissions Gap ilionyesha kuwa kujiimarisha baada ya janga la Uviko-19 kunaweza kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa kwa asilimia 25 ilivyotabiriwa kufikia mwaka wa 2030 na kuwezesha dunia kuwa karibu kufikia nyuzijoto 2 zinazolengwa chini ya Mkataba wa Paris kuhusiana na Mabadiliko ya Tabianchi.