Dodoma FM

Wakulima wakosa elimu ya upimaji wa Udongo

18 January 2024, 9:23 am

Wakulima wengi wameendelea kuvuna mazao machache kutokana na kutofuata kanuni za kufahamu afya ya udongo.Picha na Mafinga Town Blog.

Kata ya Handali ni wananchi 5 pekee ndio waliweza kukamilisha zoezi la upimaji udongo wa mashamba yao licha ya kipimo hicho kufanyika bure bila malipo katika ofisi za Wilaya ya Chamwino.

Na Victor Chigwada.

Imeeezwa kuwa wakulima wengi wamekosa elimu juu ya upimaji wa udongo hali inayo wafanya kuendelea kulima kwa mazoea bila kujali afya ya udongo.

Hayo yameelezwa na Afisa kilimo wa Kata ya Handali Bw.Daudi Kolokoni ambaye amekiri wakulima wengi wameendelea kuvuna mazao machache kutokana na kutofuata kanuni za kufahamu afya ya udongo Hata hivyo ameongeza kuwa Pamoja na changamoto hiyo bado wataendelea kuhamasisha wakulima kujenga tabia ya kupima udongo wa mashamba yao.

Sauti ya Afisa kilimo wa Kata ya Handali Bw.Daudi Kolokoni.

Kolokoni amesema kuwa endapo wakulima watakutan na changamoto ya wadudu wanao shambulia mazao yao ni vyema kufikisha taarifa hizo mara moja ofisini .

Sauti ya Afisa kilimo wa Kata ya Handali Bw.Daudi Kolokoni.

Nao baadhi ya wananchi wameshukuru kwa elimu ambayo imekuwa ikitolewa kwa wakulima juu ya kilimo chenye tija na mavuno mengi.

Sauti za baadhi ya Wananchi.

Aidha wameongeza kuwa baadhi yao wamekuwa hawana mwitikio na upimaji udongo wa mashamba yao kwa kuamini yanajitosheleza ama kuweka mbolea moja kwa moja ni suluhu

Sauti za baadhi ya Wananchi.