Dodoma FM

Tathmini ya malengo yatajwa kuwa muongozo mzuri wa kukamilisha mipango

16 January 2023, 1:54 pm

Na; Mariam Matundu.

Imeelezwa kuwa ni muhimu kufanya tathimini ya malengo au mipango yako kila wakati ili kujua iwapo mpango wako utatekelezeka hali itakayosaidia kukamilisha mipango yako kwa wakati uliupanga.

Hayo yameelezwa na mtaalamu wa masuala ya mipango Dkt George Kinyishi na kuongeza kuwa mtu anaepanga anakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya vizuri kuliko asiepanga hivyo suala la tathimini ni muhimu kila baada ya muda.

Amesema ni wakati sasa watu wajenge utamaduni wa kupanga mipango hata kwa kila siku kwani kwa sasa watu wengi wanapoteza muda bila kufanya vitu vya msingi .

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wananchi kutaka kujua ni upi wakati sahihi kwao wa kufanya tathimini ya mipango yao?

.