Dodoma FM

TAKUKURU Yaendelea kupiga vita rushwa ya ngono

2 February 2023, 1:19 pm

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo.Picha na Mwananchi

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru imesema inaendelea kupiga vita rushwa ya ngono kwani inadhalilisha utu wa Mtu.

Na Mindi Joseph

Changamoto ya rushwa ya ngono imekuwa ikiongezeka siku hadi siku kutokana na ukimya dhidi ya vitendo hivyo hali inayosababisha kuendelea kufanyika kwa siri na kuathiri wengi.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo amesema wanaendelea kukabiliana na rushwa ya ngono.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo.