Dodoma FM

RALI yaanzisha kampeni mpya ya EXCEL

16 February 2022, 3:25 pm

Na; Benard Filbert.

Shirika la RALI nchini limeanzisha kampeni mpya ya EXCEL lengo ikiwa kuitaka jamii kuchukua hatua madhubuti za kupambana na mabadiliko ya tabia za nchi kupitia utunzaji wa mazingira.

Hayo yameelezwa na afisa mradi wa taasisi hiyo bwana Elibarick Emanuel wakati akizungumza na taswira ya habari.

Amesema mradi huo unahusisha nchi tatu huku lengo kubwa ikiwa kuongeza uelewa kwa wananchi na kuchukua hatua mbalimbali zinachochangia mabadiliko ya tabia ya nchi.

Amesema mradi huo utaigusa jamii kwa kiasi kikubwa ambapo mpaka hivi sasa wamefanikiwa kuwafikia zaidi ya watu 2000.

Hata hivyo amesema jamii kubwa bado haina uelewa kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi hivyo elimu ni suala la msingi.

Shirika la RALI Tanzania limekuwa mstari wa mbele katika suala la utunzaji wa mazingira huku likijikita katika utoaji wa elimu.