Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuacha imani za kishirikina juu ya uchangiaji damu

10 March 2022, 3:14 pm

Na; Thadei Tesha.

Jamii imetakiwa kuachana na imani za kishirikina juu ya suala la kuchangia damu ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanaofariki kutokana na kukosa damu.

Akizungumza katika mahojiano maalum na kipindi cha taswira ya habari Daktari kutoka katika hospitali ya Decca dokta Methiew silayo Amesema ipo haja kwa kila mwananchi kuchangia damu ili kuokoa Maisha ya wagonjwa wanaofariki kutokana na kukosa damu.

Aidha ameongeza kuwa mahitaji ya damu yamekuwa na msaada mkubwa Nchini katika kuokoa uhai  wagonjwa  Mbalimbali katika mahospitali Nchini hivyo ni vyema wananchi kuendelea kuhamasika juu ya suala hilo.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wameshauri elimu itolewe zaidi kwa jamii juu ya umuhimu wa kuchangia damu ili kuleta hamasa zaidi kwa wananchi kwani wengi wao wamekuwa wakihusisha na imani za kushirikina.

Uchangiaji wa damu ni moja ya Jambo ambalo limekuwa likihimizwa na taasisi za afya kwa lengo la kuokoa Maisha hivyo jamii inapaswa kushirikiana kuhamasisha Jambo hilo.