Dodoma FM

Halmashauri ya jiji la Dodoma yahitimisha maadhimisho ya siku ya Afya na Lishe.  

31 March 2023, 6:21 pm

Baadhi ya wazazi walio hudhuria maadhimisho hayo. Picha na Thadei Tesha.

Maadhimisho hayo yalianza  Mwezi januari na kuhitimishwa leo Machi 31 katika hospitali ya Makole iliyopo hapa jijini Dodoma.

Na Fred Cheti.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imehitimisha maadhimisho ya siku ya afya na Lishe ya mtoto ambayo ilianza kuadhimishwa katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dodoma.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika Kituo cha afya cha Makole ambapo shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo utoaji wa elimu ya lishe ya watoto kwa wazazi kama anavyobainisha Afisa lishe wa jiji la Dodoma Bi. SemeniEva Juma

Sauti ya Afisa Lishe jiji la Dodoma
Baadhi ya wazazi walio hudhuria maadhimisho hayo. Picha na Thadei Tesha.

Miongoni mwa Elimu iliyotolewa katika maadhimisho hayo ni juu ya kuwapatia watoto vyakula ambavyo vitawapatia lishe bora ambapo hapa mtaalamu wa masuala ya lishe kituo hicho cha Makole Julieth John anafafanua.

Mtaalamu wa masuala ya lishe kituo cha Makole

Kwa upande wao baadhi ya wazazi ambao walihudhuria katika maadhumisho hayo yaliyokwenda sambamba na utoaji wa elimu ya lishe walikua na haya ya kusema.

Sauti za wazazi walio hudhuria maadhimisho hayo