Dodoma FM

Wananchi wafunguka kufuatia kauli ya Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)

28 August 2023, 12:30 pm

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambaye pia ni  Kaimu Mkurugenzi  wa Habari na Uhusiano  Makao Makuu ya Jeshi hilo, Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda, akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dodoma. Picha na Mhagalle Blog.

Ikumbukwe kuwa, Sheria ya Usalama wa Taifa  ya Mwaka 1970 kifungu cha 6, inakataza mtu yeyote ambaye hatumikii Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala jeshi lolote lililowekwa kwa mujibu wa sheria kuvaa vazi rasmi la jeshi lolote katika hayo yaliyotajwa  au vazi lolote linalofanana na vazi rasmi la majeshi hayo.

Na Abraham Mtagwa.

Wananchi Jijini Dodoma wamekuwa na maoni mbalimbali, kufuatia kauli ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyotolewa  Agost 25 ya kutoa siku saba kwa Wananchi kusalimisha mavazi ya jeshi au yanayofanana na sare za Jeshi hilo.

Wakizungumza na Taswira ya Habari baadhi ya Wafanyabiashara wa Nguo kutoka soko la Machinga Complex wamesema kuwa suala la uuzaji wa nguo hizo limekuwa ni changamoto kubwa  kuisha na hapa wanaeleza baadhi ya sababu zinazopelekea changamoto hiyo.

Sauti za baadhi ya wafanyabiashara wa nguo.
Msigwa akibadilishana mawazo na Ilonda katika mkutano huo. Picha na Mhagalle Blog.

Aidha kituo hiki kimepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya Wananchi Jijini Dodoma ambao wametoa mitazamo mbalimbali kufuatia kauli ya Jeshi hilo huku wengi wakishauri udhibiti wa nguo au sare hizo uanzie sehemu mizigo inaposhushwa kutoka nje.

Maoni ya baadh ya wananchi.

BW. Moses John, ambaye ni Mkazi wa Majengo jijini Dodoma ametoa ushauri kwa Watu wenye tabia ya kutumia Mavazi au sare za Majeshi mbalimbali Nchini kwa ajili ya kufanya  uhalifu kuacha tabia hiyo kwani inahatarisha usalama wa maisha yao na maisha yaw engine.

Sauti ya Moses John.