Dodoma FM

Uhaba wa mbegu za maboga wapunguza matumizi

22 December 2020, 12:41 pm

Na,Timotheo Chiume,

Dodoma.

Upatikanaji mdogo wa mbegu za maboga jijini Dodoma umezifanya kutotumiwa kwa wingi na watu wanaozihitaji kwa ajili ya chakula na lishe.
Pamoja na changamoto hiyo uhitaji na watumiaji wanaongezeka kila siku kutokana na kutambua faida zitokanazo na mbegu hizo.
Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wafanya biashara wa mbegu hizo jijini hapa wameelezea namna mbegu hizo zinavyopendwa na imekua faida sio tu kujipatia kipato lakini poa kwa watumiaji.

Zao la Maboga likiwa shambani

Nao wateja wa bidhaa hiyo wameelezea kutambua umuhimu wa matumizi ya mbegu za maboga kwa afya ndio maana wamekuwa wakinunua mara kwa mara.