Dodoma FM

Wizi wa mifugo washamiri Chinangali 2

2 November 2023, 11:12 am

Wizi wa mifugo, umekuwa ukirejea na kupotea kwani miaka 18 iliyopita ulizuka katika Kijiji cha Mbabala wilayani Bahi.Picha na Mindi Joseph.

Na Mindi Joseph.

Wimbi la wizi wa mifugo limeendelea kushika kasi katika Kijiji cha Chinangali 2 wilayani chamwino mkoani Dodoma ambapo Mifugo hiyo huibiwa na kuchinjwa nyakati za usiku.

Katika kipindi cha Miezi 10 ndani ya  Mwaka huu 2023 ng’ombe zaidi ya 8 wamebainika kuibiwa kijijini hapo na kuchinjwa na kuchunwa Ngozi kisha Kupelekwa buchani.

Wafugaji wanasema wezi wamekuwa wakivunja mazizi na Kuiba huku gari Ndogo zikitajwa kutumika kubebea na kusafirisha nyama zilizochinjwa usiku wa manene.

Sauti za baadhi ya wakazi wa Chinangali 2.

Wakazi wa eneo hili wanadai kuwa wizi huu wa mifugo unasababishwa na baadhi ya watu ambao ni wavivu kufanya kazi badala yake wanageuka kuiba mifugo Huku Vijana wakitiliwa mashaka ya  kujihusisha na wizi huo licha ya kuwa ushahidi bado haujapatikana.

Picha ni Mkazi wa kijiji cha Chinangali 2 akiongea na Dodoma Tv.Picha na Mindi Joseph.

Kwa mujibu wa Afisa Mifugo wa kijiji cha Chinangali 2 James Chilonwa Kijiji cha Chinangali 2 kina idadi ya ng’ombe 1250 na Mbuzi 820 na amewataka wanaojihusisha na wizi wa Mifugo kuacha mara moja.

Sauti ya Bw. James Chilonwa.

Wizi wa mifugo, umekuwa ukirejea na kupotea kwani miaka 18 iliyopita ulizuka katika Kijiji cha Mbabala wilayani Bahi ambapo Ngo’mbe 84 na nguruwe 36 walitajwa kuibiwa na kuchangia kufanyika Msako mkali  mwaka 2002 hadi 2004 kukomesha vitendo hivyo.