Dodoma FM

Halmashauri ya jiji la Dodoma yapanga kushirikiana na wadau kuongeza ufaulu

27 March 2023, 5:46 pm

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh. Jabir Shekimweri akizungumza katika mkutano huo. Picha na Fred Cheti.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma lazima iwe mfano kwa kushika nafasi ya juu katika elimu na si elimu tu hata kwenye mambo mengine.

Na Fred Cheti.

Halmashauri ya jiji la Dodoma imepanga kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu jijini hapa ili kuboresha sekta ya elimu ikiwemo kuongeza ufaulu wa wanafunzi .

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh. Jabir Shekimweri katika kikao cha halmashauri ya jiji pamoja na wadau wa elimu kilichokuwa na lengo la kuweka mikakati ya uboreshaji wa elimu katika jiji la Dodoma.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mh. Jabir Shekimweri .
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bwana Joseph Mafuru .Picha na Fred Cheti.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bwana Joseph Mafuru amesema halmashauri ya jiji la Dodoma ni lazima iwe ya mfano kwa kuongoza katika sekta zote ikiwemo elimu hususani suala la ufaulu wa wanafunzi.

Sauti ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Mh. Joseph Mafuru.

Nao Maafisa elimu Msingi na Sekondari katika jiji la Dodoma walikuwa na haya ya kuzungumza Juu ya mikakati ya kuboresha ufaulu wa wanafunzi katika jiji la Dodoma.

Sauti za Maafisa elimu Msingi na Sekondari katika jiji la Dodoma