Dodoma FM

Waandishi wa habari watakiwa kutoa taarifa sahihi

26 March 2024, 6:42 pm

Picha ni Bw. Richard Msittu Mkuu wa ofisi za Kanda Taasisi ya Sikika Jijini Dodoma.Picha na Mariam Kasawa.

Mlipuko wa magonjwa unapotokea waandishi wa habari ni nyenzo muhimu ya kutoa taarifa sahihi.

Na Mariam Matundu.
Waandishi wa habari wametakiwa kuhakikisha usahihi wa Taarifa ili kuepusha taharuki kwa jamii wakati wa magonjwa ya Mlipuko.

Hayo yamebainisha Richard Msittu Mkuu wa ofisi za Kanda Taasisi ya Sikika Jijini Dodoma katika mafunzo yaliyowakutanisha waandishi wa habari.

Amesema Mlipuko wa magonjwa unapotokea waandishi wa habari ni nyenzo muhimu ya kutoa taarifa sahihi.

Sauti ya Richard Msittu.

Kwa pande wake Grace Msemwa kutoka Wizara ya Afya amesema katika magonjwa ya mlipuko yanapotokea wanashirikiana na wizara zote kukabilia na ugonjwa huo.

Sauti ya Grace Msemwa kutoka Wizara ya Afya.