Jamii yatakiwa kuzingatia matumizi ya chakula salama
4 June 2026, 18:42

Wiki ya chakula salama uadhimishwa kuanzia tarehe 1 June hadi tarehe 7 June kila mwaka,na mwaka huu imeambatana na kauli mbiu inayosema kuwa,kutoka katika changamoto kuelekea suruhisho chakula salama kila mahali.
Na Jerome John.
Kuelekea kilele cha wiki ya chakula salama Duniani jamii imetakiwa kuhakikisha inatumia chakula salama kuanzia shambani mpaka mlaji wa mwisho.
Wito huo umetolewa na Vicent Tarimo Afisa Mdhibiti Ubora Mwandamizi shirika la viwango Tanzania, akizungumza na Taswira ya habari katika kutoa elimu ya matumizi ya chakula salama katika jamii na madhara ya utumiaji wa chakula kisicho salama.
Afisa huyo amesema kuwa chakula salama ni kile ambacho kimezalishwa na kuandaliwa katika mazingiora bora yaliyozingatia kanuni za ubora na kutoleta madhara ya kiafya kwa mlaji yakiwemo magonjwa.
Aidha ameeleza kuwa usalama wa chakula unaambatana na mazingira yote ambayo mtu hupata chakula iwe vyakula vya kusindikwa kutoka viwandani au visivyo vya viwandani muhimu ni mnyororo wote wa uzalishaji chakula mfano kuanzia kwa mkulima,mfugaji,mvuvi,msafirishaji hadi kwa mlaji.
Vile vile amebainisha kuwa chakula kinaweza kuhathiriwa na bacteria,virusi au fangasi na kusababisha magonjwa kama saratani kwa binadamu pamoja na magonjwa ya figo na mengineyo na hapo kunakuwa hakuna ubora,na kusisitiza kuwa vyakula vyote vinavyofungashwa vinatakiwa kuwa katika vifungashio bora na salama.