

10 June 2025, 1:44 pm
Licha ya serikali kuruhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kipindi cha masomo kurejea Shule Lakini bado kumekuwa na changamoto lukuki.
Na Kitana Hamis.
Wadau wa Elimu wataka Mongozo wa Serikali kwa Wanafunzi wa Kike walio Pata Ujauzito kurejea Shule ili watimize ndoto zao.
Akizungumza wakati wa wiki ya azaki 2025 Dr wilifipa fosi mena Mshauri wa kiufudi Elimu kutoka taasisi ya haki elimu Pamoja na Wadau mbali mbali kutoka asasi za kiraia wamesema licha ya Serikali kuruhusu wanafunzi wanaopata Ujauzito kipindi Cha masomo kurejea Shule Lakini bado kumekuwa na changamoto lukuki zinazowakabili wanafunzi hao kutorejee Shule kutokana na Mazingira yao kuwa magumu.
Noriya Mshale mtaalamu wamaswaala ya njisia na Maendeleo Kutoka taasisi ya haki ya Elimu Pamoja na frolesi ng,ari mtafiti wamaswaala ya Elimu kutoka taasisi hio hapa wanaiomba Serikali kuweka Mazingira wezeshi na yenye usawa iliwanafuzi wakike walio katisha masomo yao kurejea Shule kwalengo la kutimiza ndoto zao.