Dodoma FM

Vijana Kiteto waaswa kutotegemea urithi wa wazazi

5 June 2026, 17:04

Vijana wengi wana uwezo mkubwa wa kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo, lakini changamoto kubwa imekuwa ni baadhi yao kukata tamaa na kusubiri kupata ajira au urithi.Picha na Kitana Hamis.

Viongozi wa dini wana wajibu wa kuendelea kuwahimiza vijana kuzingatia maadili mema.

Na Kitana Hamis.

Vijana wilayani Kiteto mkoani Manyara wameaswa kuacha kutegemea urithi kutoka kwa wazazi wao na badala yake kujikita katika kufanya kazi kwa bidii, kujiajiri pamoja na kutumia vizuri vipaji walivyonavyo ili kujenga maisha bora.

 Kijana Adamu Rashidi ambaye ni fundi wa majiko ya vyakula ya kisasa wilayani Kiteto mkoani Manyara, amewataka vijana kuacha kutegemea urithi au msaada wa watu wengine pekee na badala yake kujikita katika kufanya kazi kwa bidii, kujiajiri pamoja na kutumia vizuri vipaji walivyonavyo ili kujenga maisha bora na yenye mafanikio.

Adamu amesema kuwa vijana wengi wana uwezo mkubwa wa kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo, lakini changamoto kubwa imekuwa ni baadhi yao kukata tamaa na kusubiri kupata ajira au urithi pekee badala ya kutumia fursa zilizopo katika jamii kujiongezea kipato na kujitegemea.

Kwa upande wake, kiongozi mmoja wa dini wilayani kiteto amesema vijana wanapaswa kumtanguliza Mungu katika maisha yao, kuwa na nidhamu, uadilifu na moyo wa kufanya kazi kwa bidii kwani mafanikio ya kweli yanahitaji uvumilivu na juhudi za halali.

Amesema viongozi wa dini wana wajibu wa kuendelea kuwahimiza vijana kuzingatia maadili mema, kujiepusha na vitendo viovu pamoja na kutumia muda wao katika shughuli za maendeleo zitakazowasaidia wao binafsi, familia zao na jamii kwa ujumla.

Sauti ya Kitana Kina