Dodoma FM
Dodoma FM
27 April 2026, 13:23

Muhuri amewataka Wananchi kutumia fedha hizo Kwa manufaa ili waweze kubadilisa maisha yao na kuanza kuishi Kwa kujitegemea.
Na Victor Chigwada.
Wanufaika na walengwa wa mfuko wa kusaidia kaya masikini TASSAF katika kijiji cha Msamalo wameishukuru serikali kupitia mfuko huo kwani umesaidia kuboresha maisha yao.
Wakiongea na Taswara ya habari wanufaika wa mfuko huo Kata ya Msamalo Wilaya ya Chamwino wamesema kupitia mfuko huo wameweza kufanya shughuli mbalimbali za kuwaingiazia kipato na kujikwamua kiuchumi.
Aidha wameiomba serikali kuendelea kuwasaidiakupitia mfuko huo pamoja na kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu .
Bi. Ng’washi Muhuri afisa maendeleo wa Kata ya Msamalo amesema licha ya fedha hizo kutolewa kwa makundi yaliyo kusudiwa lakini baadhi ya watu wameshendwa kuzitumia pesa hizo kwa usahihi badala yake wanaishia kuzitumia vibaya ikiwa ni pamoja na kulewa pombe.