Dodoma FM
Dodoma FM
28 April 2026, 14:20

Utoaji wa elimu hiyo ni sehemu ya mkakati wa Jiji la Dodoma kuhakikisha shule zinabaki kuwa maeneo salama kwa watoto ili waweze kutimiza ndoto zao bila hofu.
Na Mariam Kasawa.
Katika mwendelezo wa kampeni ya kulinda haki na usalama wa watoto, leo tarehe 28, Aprili, 2026 Polisi Wilaya ya Dodoma imetoa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Mnadani, Chihoni na Nala mapema leo.
Lengo la elimu hiyo ni kuwajengea uelewa wanafunzi kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji na unajisi pamoja na kuwaelekeza mbinu za kujikinga na muhimu zaidi hatua za kuchukua na sehemu sahihi za kuripoti wanapokutana na viashiria vya vitendo hivyo.