Dodoma FM
Dodoma FM
10 October 2024, 19:00

Na Mariam Kasawa.
Kampuni ya mikopo ya Enterprice Financial Limited EFL imechagiza kauli mbiu ya Dodoma ya Kijani kwa kupanda miti katika maeneo ya Kndege Shule ya Msingi iliyopo jijini Dodoma.
Meneja wa ampuni hiyo ya EFL tawi la Dodoma Bwn. Niwakoel Ndosa amesema wameamua kuunga mkono kaulimbiu ya Dodoma ya Kijani kwa kupanda miti katika Shule ya Msingi K ndege ikiwa ni sehemu ya kurejesha kwa jamii.

Muhifadhi Mkuu kutoka wakala wa misitu Tanzania TFS Bi. Husna Msagati amesema miti hiyo inapaswa kutunzwa ili kutimiza kauli mbiu ya Dodoma ya kijani.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kndege amesema amefurahishwa na zoezi hilo la upandaji miti kwani limesaidia wanafunzi kushiriki kwa vitendo elimu ya utunzaji mazingira.

Zoezi hilo la upandaji miti lililofanyika shuleni hapo mapema leo hii limehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakala wa misitu Tanzania TFS, NEMC, mwenyekiti wa mtaa , Diwani wa Kata ya Kndege. pamoja na wanafunzi.
