Dodoma FM

Vijana watakiwa kutumia fursa zinazojitokeza kujikwamua kiuchumi

22 June 2023, 5:01 pm

Mwenyekiti mtendaji wa shirika lisilo la Kiserikali la KLNT Bw.Isaac Mpatwa akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Rabiamen Shoo.

Shirika la Kingdom Leadership Network Tanzania(KLNT) limekuwa likiratibu mikutano ya maombi kwa Taifa ikifahamika kama Tanzania Prayer Breakfast.

Na Rabiamen Shoo.

Wananchi hususan vijana wametakiwa kuzitumia vizuri fursa zinazojitokeza katika maeneo yao kupata elimu hususan namna ya kufanikiwa kiuchumi.

Wito huo umetolewa hii leo jijini Dodoma na mwenyekiti mtendaji wa shirika lisilo la Kiserikali la KLNT Bw.Isaac Mpatwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.

Mpatwa amesema kuwa mbali na mkutano huo kuwa wa fursa kwa vijana lakini utakuwa na malengo mengine matatu.

Sauti ya mwenyekiti mtendaji wa shirika lisilo la Kiserikali la KLNT .

Aidha Mpatwa amesema kuwa kutakuwa na wanenaji kutoka ndani na nje ya nchi ambao anawataja:

Sauti ya mwenyekiti mtendaji wa shirika lisilo la Kiserikali la KLNT .
Dr.Canon Mosses Matonya ambaye ni katibu mkuu wa baraza la Kikristo Tanzania akiongea katika mkutano huo na waandishi wa habari . Picha na Rabiamen Shoo.

Katika mkutano huo Bilionea kutoka nchini Marekani  Llyod Ward atakuwa akiwafundisha vijana namna ya kufanikiwa katika shughuli zao zikiwemo  kibiashara kama anavyosema Geofrey Simbeye ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa Taasisi ya sekta binafsi TPSF ambae pia ni Mkurugenzi mkazi wa Ward Holdings International.

Sauti ya mwenyekiti mstaafu wa Taasisi ya sekta binafsi TPSF.

Naye mchungaji Dr.Canon Mosses Matonya ambaye ni katibu mkuu wa baraza la Kikristo Tanzania amesema kuwa kinachotakiwa ni elimu ya kutosha ili kupata maarifa ya kutawala na kutunza vitu vyetu.

Sauti ya katibu mkuu wa baraza la Kikristo Tanzania.