Dodoma FM

Wazazi Mbwanga wahimizwa kusimamia malezi kukomesha utoro

31 May 2023, 1:17 pm

Wananchi wa Mtaa wa Mbwanga wakiwa katika mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alipo fanya ziara katika eneo hilo. Picha na Fred Cheti.

Wananchi wamehimizwa pia kuendelea kutunza mazingira kwa kushiriki katika upandaji miti.

Na Fred Cheti.

Wazazi wa mtaa wa Mbwanga kata ya Mnadani mkoani Dodoma wamehimizwa kusimama vizuri katika malezi ya watoto ili kupunguza utoro wa wanafunzi unaotajwa kukithiri kwenye baadhi ya shule katika kata hiyo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule wakati akizungumza na wananchi hao  baada ya kufanya ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa  shule ya Msingi Mbwanga unaojengwa katika mtaa huo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma

Katika hatua nyingine Mhe. Rosemary amewahimiza wananchi katika mtaa huo kuendelea kutunza mazingira ikiwemo kushirikia katika upandaji miti hasa katika maeneo yao ya makazi na biashara.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma pamoja na wajumbe wengine wakikagua ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Mbwanga. Picha na Fred Cheti.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe Godwin Gondwe amewapongeza wananchi wa mtaa huo kwa ushiriki wao wa hali na mali katika kushirikiana na serikali kufanikisha ujenzi wa shule hiyo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Bahi