Dodoma FM

Jumuiya ya wazazi CCM Bahi yalaani ndoa za jinsia moja

28 April 2023, 2:00 pm

Yohana Mgomi Mwenyekiti Wazazi wilaya ya Bahi. Picha na Bernadi Magawa.

Maadhimisho hayo yalianza kwa kutoa elimu ya malezi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari  Bahi  ambapo wanafunzi walisisitizwa kuhusu nidhamu na bidii katika masomo.

Na Bernad Magawa.

Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Bahi imetoa tamko la kulaani vikali ndoa za Jinsia moja na kuwashauri wazazi na walezi kukazia suala la malezi katika familia ili kuwa na taifa lenye hofu ya Mungu na maadili bora.

Tamko hilo limetolewa na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo wilaya ya Bahi Yohana Mgomi  katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya wazazi wilaya ya Bahi yaliyofanyika katika ofisi za ccm  wilayani humo hapo jana.

Sauti ya Yohana Mgomi – Mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Bahi.
Shufaa Saidi – Mjumbe baraza la Wazazi Wilaya ya Bahi akitoa elimu kwa wanafunzi. Picha na Bernadi Magawa.

Akizungumza katika maadhimisho hayo katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Bahi Paulina Bupamba amewaasa wazazi  kukemea mambo yote yanayoharibu maadili ya watoto na kuhakikisha watoto wanapata haki yao ya  elimu.

Sauti ya Paulina Bupamba katibu wa CCm wilaya ya Bahi.

Awali maadhimisho hayo yalianza kwa kutoa elimu ya malezi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari  Bahi  ambapo wanafunzi walisisitizwa kuhusu nidhamu na bidii katika masomo na baadae kuendelea na elimu mbalimbali ambapo viongozi wengine na wanachama wakaeleza mambo mbalimbali.

Sauti za Wanachama na viongozi mbalimbali.