Dodoma FM

CAG, TAKUKURU Zaagizwa kufanya uchunguzi BOT

29 March 2021, 5:55 am

Na; Mariam Kasawa.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kushirikiana kwa pamoja kuchunguza fedha zilizotoka Benki kuu ya Tanzania kwa kipindi cha Januari mpaka Machi 2021.

Rais Samia amefikia uamuzi huo  Machi  28, 2021 baada ya kusomewa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Takukuru Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Amesema ijapokuwa katika mashirika ya umma hakuna hati mbaya, lakini kumekuwa na upotevu mkubwa wa fedha jambo ambalo linahitaji kushughulikiwa.

Ametoa tamko  kwa Takukuru, na  Gavana wa benki kupitia  fedha zote zilizotoka katika kipindi cha Januari mpaka Machi mwaka huu, zilizokwenda kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.