Dodoma FM

Rasimu mkakati wa kilimo ikolojia yatakiwa kuwa katika lugha rahisi

26 September 2023, 3:57 pm

Wadau wa kilimo ikolojia hai wakiwa katika mkutano huo jijini Dodoma. Picha na David Kavindi.

Kongamano hilo limejumuisha wadau wa kilimo na wakulima kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania mkakati wa kilimo hai unatarajia kuja na majibu juu ya kilimo hai .

Na David Kavindi.

Imeelezwa kuwa rasimu ya mkakati wa kilimo ikolojia hai inatakiwa kufanyiwa marekebisho ili iwe katika  lugha rahisi itakayoeleweka kwa wakulima  .

Hayo yamesemwa na  mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo chini Bw. Obadiah Nyegiro ambapo ameyasema kuwa hayo katika uzinduzi wa kongamano la kilimo hai ikolojia ulilofanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Morena hotel ambapo amewataka wadau  wanaosimamia mkakati wa kilimo ikolojia hai kuzingatia lugha rahisi itakayoeleweka kwa wakulima kwa ajili ya utekelezaji. 

Sauti ya Bw. Obadia Nyegiro.
Picha ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo nchini Bw. Obadiah Nyegiro akizungumza katika Mkutano huo. Picha na David Kavindi.

Naye mwenyeketi wa kamati ya uandaaji wa kamati ya  taifa  ya kilimo  ikolojia hai  Bw. Levelen Ngaiza ameeleza malengo ya mkakati huo ni kuhakikisha kama Taifa linazalisha chakula  na kuzingatia kulinda mazingira

Sauti ya Bw. Levelen Ngoiza.

Nao baadhi ya wadau na wakulima wa kilimo hai walioshiriki katika kongamano hilo wameiomba serikali kusimamia mkakati wa kilimo hai na kuongeza elimu juu ya makakati huo na kuongeza teknolojia iliku kusaidia wakulima wadogo kupata pemebejeo za kisasa

Sauti ya mdau wa kilimo hai.