Dodoma FM

Watakiwa kuwa waaminifu michango ya shule shikizi

9 June 2026, 17:33

Wananchi waamua kuanzisha ujenzi wa shule shikizi kwa nguvu zao wenyewe.Picha na Mtandao.

Wananchi wapo tayari kuanza zoezi la kuchangia na kujenga shule kwa kuliwekea utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa michango.

Na Victor Chigwada.

Kuelekea zoezi la kuchangia ujenzi wa shule shikizi katika kitongoji cha Ilolo mtaa wa Ihumwa A wito umetolewa kwa mabalozi wa nyumba kumi kuwa waaminifu wakati wa ukusanyaji wa michango ya ujenzi wa shule hiyo kutoka kwa wananchi.

Hayo yanafuatia baada ya wananchi kuamua kuanzisha ujenzi wa shule shikizi kwa nguvu zao wenyewe ili kuwasogezea watoto wao huduma ya shule karibu wakiongea na taswira ya habari wamesema wanawaomba viongozi watao husika kukusanya michango kutoka kwa wananchi wawe waaminifu ili zoezi hilo lifanikiwe.

Sauti za wananchi

Lameki Mbinda mwenyekiti wa mtaa huo amesema kuwa wapo tayari kuanza zoezi hilo na wataliwekea utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa michango ili kusiwepo  na upotevu wowote wa pesa.

Sauti ya Lameki Mbinda

Nae mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Ihumwa ambae pia ni msimamizi wa mabalozi wa mabalozi wa nyumba 10  Bw.John Kusaduka ameahidi kulifanyia kazi huku akiwataka mabalozi hao kuwa waaminifu katika shughuli za kijamii.

Sauti ya Bw.John Kusaduka