Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuwa na utaratibu wa kupima afya kila wakati

1 July 2026, 16:57

Idara ya Afya inapaswa kuongeza uhamasishaji kwa jamii ya kupima afya mara kwa mara.Picha na Mtandao.

Kwa upande wake, mkazi wa Mpwapwa, Bi. Dorin Mbilinyi, amesema wananchi wengi hasa wa vijijini bado hawana uelewa wa kutosha juu ya upimaji wa afya.

Na Stephen Noel.

Jamii Wilayani  Mpwapwa  mkoni Dodoma imehimizwa kuwa na utaratibu wa kupima afya mara kwa mara ili kujikinga na madhara yanayotokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Rai hiyo imetolewa  na Mganga wa Magonjwa ya Ndani , Dkt. Fransica Komanya, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Akifafanua, Dkt. Komanya amesema magonjwa kama shinikizo la damu, kisukari na saratani ndio vyanzo vikuu vya vifo nchini, lakini kwa bahati mbaya hayana dalili za mapema.

Mganga huyo amesema mabadiliko ya mtindo wa maisha ndio yamesababisha ongezeko la magonjwa hayo siku hadi siku.

Sauti ya Noel kina