Kesi migogoro ya ardhi zaongoza Kondoa kampeni ya msaada wa kisheria
18 May 2026, 17:42

Kampeni hiyo imeratibiwa na serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kwa lengo la kutoa msaada wa kisheria bure kwa wananchi.
Na Bennard Komba.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inayo ratibiwa na Wizara ya Katiba na Sheria imefanikiwa kupokea migogoro zaidi ya 140 katika kipindi cha siku 15 za utekelezaji wa kampeni hiyo katika Halmashauri ya Mji Kondoa mkoani Dodoma, huku migogoro mingi ikiwa ni ya ardhi.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Everett Magile Stephen, alipokuwa akizungumza na Dodoma FM baada ya kukamilika kwa awamu ya pili ya kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC).
Amesema kampeni hiyo ilianza Mei 1, 2026 na kufanyika katika kata 8 pamoja na mitaa 36 ya Halmashauri ya Mji Kondoa, ikiwa na lengo la kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa jamii katika masuala mbalimbali ikiwemo migogoro ya ndoa, mirathi, ardhi, matunzo ya watoto pamoja na ukatili wa kijinsia.
Akizungumzia mafanikio ya kampeni hiyo, amesema imefanikiwa kuwafikia wananchi zaidi ya 45,000, idadi ambayo ni zaidi ya nusu ya wakazi wote wa Halmashauri ya Mji Kondoa.
Aidha, ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kushiriki katika kampeni hiyo, ambapo umeweza kutatua changamoto mbalimbali zinazo husiana na mafao ya wanachama, jambo lililo waletea faraja wananchi waliokuwa wakikabiliwa na changamoto hizo.
Pia ametoapongezikwaofisiyahalmashauriyamjiwaKondoa,ofisiyamkuuwa wilaya Pamoja nakituo cha polisiDawati la jinsianawatotokwakuwezeshakampenihiyo
Kwa upande wao, wananchi wamepongeza ujio wa awamu ya pili ya kampeni hiyo huku wakiiomba serikali kuendelea kuitekeleza mara kwa mara ili kusaidia kupunguza migogoro mbalimbali inayotokana na uelewa mdogo wa masuala ya kisheria.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) ilianza rasmi Mei 1, 2026 katika wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na kuhitimishwa Mei 15, 2026.