Dodoma FM

Wazazi acheni kushinikiza watoto wajifelishe.

15 March 2022, 1:40 pm

Na;Mindi Joseph .                                    

Wazazi Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wametakiwa kuachana na tabia ya kuwashinikiza watoto kujifelisha katika masomo yao.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Elimu Michezo Wilayani humo Nicholaus Achimpota ambapo amesema hali hiyo inapelekea kurudisha nyuma maendeleo ya elimu wilayani humo.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Mipango Fedha na Utawala, Vedastus Timothy amesema wataendelea kuwahimiza watoto kusoma kwa bidii zaidi licha ya changamoto anazokumbana nazo.

Amewataka wananchi kuunga mkono elimu  kwani kufanya hivyo itakuwa chachu kwa  wanafunzi shuleni kusoma kwa bidii na hatimaye kutimiza malengo yao waliyojiwekea.