Dodoma FM

WEO, VEO watakiwa kuhakikisha watoto wote wanawasili shuleni

9 January 2024, 8:10 am

Picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Rosemery Senyamule akiongea katika ziara yake hiyo. Picha na Thadei Tesha.

Mkuu wa mkoa ametembelea baadhi ya shule ikiwemo shule mpya ya sekondari miyuji pamoja na shule ya msingi Chikoye iliyopo msalato jijini Dodoma.

Na Thadei Tesha.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh Rosemery Senyamule amewaagiza watendaji wa kata na mitaa kuhakikisha ndani ya  wiki hii watoto wote wanaotakiwa kujiunga na masomo wawe wameshawasili shuleni.

Wakati Wanafunzi kote Nchini wakianza masomo yao kwa mwaka huu hii leo mkuu wa mkoa wa Dodoma anafanya ziara ya kukagua mwitikio wa wananfunzi waliowasili shuleni ambapo ameoneshwa kuridhishwa na mwitikio wa mahudhurio kwa baadhi ya shule huku baadhi mahudhurio yakiwa ya wastani na kuridhisha.

Picha ni wanafunzi wakiwa darasani wakati wa ukaguzi huo. Picha na Thadei Tesha.

Hapa Mkuu wa mkoa wa Dodoma anatumia fursa hii kuzungumza na watendaji wa kata na mitaa juu ya kuhakikisha wananfunzi wote waliopo majumbani wanafika shuleni ndani ya wiki hii.

Sauti ya Mh. Rosemery Senyamule.

Baadhi ya viongozi walio ambatana na mkuu wa mkoa katika ziara ya kukagua  shule hizo akiwemo mkuu wa wilaya ya dodoma mjini pamoja na meya wakawa na haya ya kuzungumza.

Sauti za Mh. Jabir Shekimweri na mh Davis Mwamfupe.