Dodoma FM

Serikali yaendelea kuboresha mazingira ya Tehama katika elimu.

24 July 2026, 15:53

Picha ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Mh. Angellah Kairuki alipotembelea shule ya msingi Mlembule wilayani Mpwapwa.Picha na Anwary Shaban.

Ndani ya kipindi cha miaka mitano serikali imefanikiwa kujenga shule 12 zenye thamani ya takribani shilingi bilioni 15.1 katika Wilaya ya Mpwapwa.

Na Anwary Shaban.

Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya Tehama katika elimu kwa kuongeza vifaa vya ufundishaji na ujifunzaji shuleni ili kuboresha maendeleo ya elimu nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Mh. Angellah Kairuki alipotembelea shule ya msingi Mlembule wilayani Mpwapwa alipo kuwa akiweka jiwe la msingi katika shule hiyo ambapo ameahidi kuipatia shule hiyo kompyuta kwaajili ya kujifunzia.

Mhe. Kairuki amesema ndani ya kipindi cha miaka mitano serikali imefanikiwa kujenga shule 12 zenye thamani ya takribani shilingi bilioni 15.1 katika Wilaya ya Mpwapwa.

Amesema pia serikali wilayani humo tayari imekwisha jenga madarasa 251 ,mabweni 11 pamoja na matundu ya vyoo 265 hatua inayolenga kuboresha huduma za elimu na kuongeza mazingira bora ya kujifunzia.

Picha ni wakazi wa kata ya Mlembule wilayani Mpwapwa wakiwa katika mkutano na waziri kairuki shuleni hapo. Picha na Anwary Shaban.

Aidha mkuu wa mkowa wa Dodoma amemshukuru mh.Angellah Kairuki kwa kitendo cha kuridhia na kuahidi kujengwa kwa darasa la Tehama na kuleta vifaa vya kujifunzia  ili kuleta usawa wa elimu.

Nae mbunge wa mpwapwa Mhe,George Malima amesema ujio wa waziri Kairuki katika shule umeleta ahueni kwani hapo awali shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na changamoto nyingi ambapo kwasasa zitakwenda kutatuliwa.

Sauti ya Anwary.