Dodoma FM

Mbinu mbadala zitumike kupandisha ufaulu wa wanafunzi

10 September 2026, 17:10

Wazazi na walimu, pamoja na kufuatilia maendeleo ya watoto na kuwasaidia pale wanapokabiliwa na changamoto za masomo.Picha na mtandao.

Mwalimu Shabani amewataka wazazi kuwaunga mkono walimu kwa kuwapa watoto muda wa kutosha wa kujisomea wanaporudi nyumbani, pamoja na kuhakikisha wanahudhuria vipindi vya ziada bila kukosa, ili mikakati hiyo iweze kuleta matokeo chanya katika ufaulu wao.

Na Derick Mazemba.

Hatua za makusudi na za haraka zimetajwa kuwa muhimu katika kukabiliana na kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi, huku shule zikitakiwa kubaini changamoto zinazosababisha hali hiyo na kuweka mikakati ya kuzitatua ili kuboresha maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi.

Baadhi ya wazazi wanaofuatilia maendeleo ya watoto wao wamesema kupanda kwa ufaulu kunahitaji ushirikiano wa karibu kati ya wazazi na walimu, pamoja na kufuatilia maendeleo ya watoto na kuwasaidia pale wanapokabiliwa na changamoto za masomo.

Akizungumzia mikakati inayotumika shuleni pale ufaulu unaposhuka, Mkuu wa Shule ya Msingi Mlangwa B iliyopo Kata ya Mpunguzi jijini Dodoma, Mwalimu Shabani Mussa, amesema wamekuwa wakitoa muda wa ziada wa kufundisha baada ya vipindi vya kawaida, ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa mada ambazo hawakuzielewa vizuri.

Aidha, amesema wanafunzi wamegawanywa katika makundi kulingana na uwezo wao darasani, hatua inayowawezesha walimu kutoa msaada wa karibu kwa wanaohitaji uangalizi maalum.

Sauti na Derick Mazemba.