Dodoma FM

‘Kitchen party’ zaibua mjadala kuhusu maadili

9 September 2026, 16:53

Mabadiliko ya jamii na utandawazi pia ni miongoni mwa mambo yanayochangia mabadiliko ya baadhi ya maadili. Picha na mtandao.

Mkufunzi wa sherehe za kunfundisha binti Bi,Hawa Ramadhani amesema mafundisho yanayotolewa katika sherehe hizo yanalenga kumjenga mwanamke kuwa bora na mwenye uwezo wa kutekeleza majukumu yake katika familia, akibainisha kuwa mabadiliko ya jamii na utandawazi pia ni miongoni mwa mambo yanayochangia mabadiliko ya baadhi ya maadili.

Na Daniel Njau.

Sherehe za maandalizi ya ndoa maarufu kama kitchen party, zinazolenga kumuandaa au kumuaga binti kabla ya kuingia kwenye ndoa, zimeibua mjadala miongoni mwa jamii kuhusu baadhi ya mafundisho na vitendo vinavyofanyika katika sherehe hizo, huku baadhi ya wananchi wakivitazama kuwa vinaweza kuchangia mmomonyoko wa maadili.

Baadhi ya wananchi wamesema hawana uelewa wa kutosha kuhusu shughuli hizo, huku wengine wakisema wamekuwa wakizisikia na kutofurahishwa na baadhi ya mambo yanayofanyika. Hali hiyo imeibua mjadala kuhusu iwapo mafundisho yanayotolewa yanaendana na lengo la kujenga familia bora na kuimarisha maadili katika jamii.

Sauti na Daniel Njau.