Dodoma FM

Adhabu kali humfanya mtoto kuwa na hofu

26 August 2026, 17:20

Adhabu kali inaweza kumjengea mtoto hofu na kumfanya ashindwe kujiamini.Picha na mtandao.

Amewashauri wazazi kuwa karibu na watoto wao na kuzungumza nao kwa upendo ili kujenga uaminifu, jambo litakalo wawezesha watoto kueleza changamoto zao na kusaidiwa mapema.

Na Rahel Joseph.

Imeelezwa kuwa adhabu kali kwa mtoto humjengea hofu na kumfanya ashindwe kujiamini  na kueleza changamoto wanazo pitia.

Baadhi ya wazazi jijini Dodoma wanasema adhabu sio njia  kwani  inaweza kuwafanya watoto kuishi kwa hofu, kushindwa kueleza changamoto wanazopitia na hatimaye kuficha makosa yao badala ya kujifunza .

Aidha baadhi ya wazazi wamesema  mtoto anapokabiliwa na adhabu kali anapopata changamoto, anaweza kuogopa kurudi kwa mzazi na kutoa taarifa, hali inayoweza kuongeza madhara ya tatizo.

Madam Muhere ni mshauri wa malezi na masuala ya familia,kutoka jijini Dodoma yeye anasema  adhabu kali inaweza kumjengea mtoto hofu na kumfanya ashindwe kujiamini, hivyo wazazi wanapaswa kutumia adhabu zenye manufaa kwa mtoto, ikiwemo kumuelekeza na kumfundisha kutambua makosa yake.

Sauti ya Rahel