Watoto wafundishwe kuepuka utegemezi wa kila kitu kwenye teknolojia
2 September 2026, 16:43

Nchini Tanzania, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeweka National Digital Education Strategy 2025–2030 pamoja na miongozo ya elimu ya kidijitali na matumizi ya AI katika elimu.
Na Crispine Gerald.
Imeelezwa kuwa ni muhimu kuwafundisha watoto namna ya kutumia teknolojia kwa usalama, kutambua taarifa zisizo sahihi na kutumia AI kama chombo cha kujifunzia badala ya kutegemea teknolojia kufanya kila kitu.
Teknolojia ya akili bandia maarufu kama AI, pamoja na ujuzi wa kidijitali, imeendelea kuwa sehemu ya maisha na elimu , je kuna umuhimu wa kuwafundisha watoto misingi ya matumizi salama na sahihi ya teknolojia wakiwa bado shuleni?
Baadhi ya wazazi wanasema ni muhimu watoto kujifunza ujuzi wa kidijitali na misingi ya AI mapema ili iweze kuwasaidia katika masomo yao na kutatua mambo mbalimbali.
Cyprian Typhone ni mtaalamu wa teknolojia toka chuo kikuu cha Dodoma yeye anasema ni muhimu watoto kuanza kujifunza misingi ya akili unde na digital skills mapema, kwa kuzingatia umri wao.
Anasema elimu hiyo inapaswa kuwafundisha namna ya kutumia teknolojia kwa usalama, kutambua taarifa zisizo sahihi na kutumia AI kama chombo cha kujifunzia badala ya kutegemea teknolojia kufanya kila kitu.
Kwa mujibu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa(UNESCO) linapendekeza wanafunzi wajenge uelewa kuhusu AI, maadili, matumizi salama na uwezo wa kutathmini kwa kina taarifa zinazotolewa na mifumo ya AI. INSERT…….. MTAALAMU WA TEKNOLOJIA