Dodoma FM

Wanandoa watakiwa kusikilizana kuepusha vitendo vya ukatili

2 September 2026, 16:16

Ni vyema jamii kuondokana na maisha ya vipigo ndani ya ndoa kwani ni unyanyasaji wa kijinsia.Picha na Mtandao.

Upo umuhimu wa matukio hayo kuchukuliwa hatua stahiki yanapo ripotiwa kwani baadhi ya watu licha ya kutoa taarifa za ukatili.

Na Victor Chigwada.

Wito umetolewa Kwa wanandoa kuhakikisha wanaishi maishi ya kusikilizana na mapatano badala ya kutumia adhabu kurebishana au kuchukua maamuzi ya kutumia pombe kuondoa mawazo.

Hayo yameelezwa na Inspector Kutega  polisi Kata ya Ihumwa wakati akitoa elimu Kwa wananchi na kuwataka wanandoa kutumia lugha moja kulinda amani ya maisha yao ya ndani .

Kutega ameongeza kuwa ni vyema jamii kuondokana na maisha ya vipigo ndani ya ndoa kwani ni unyanyasaji wa kijinsia .

Nao baadhi ya wananchi wamesema upo umuhimu wa matukio hayo kuchukuliwa hatua stahiki yanapo ripotiwa kwani baadhi ya watu licha ya kutoa taarifa za ukatili lakini bado wamekuwa hawaoni utatuzi wa kesi hizo.

Sauti ya Victor.