Vijana watakiwa kutumia kilimo kujiajiri ili kuongeza kipato
8 September 2026, 16:52

Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) na Benki ya Dunia, kilimo ni chanzo muhimu cha maisha kwa Watanzania wengi na kilichangia asilimia 25.9 ya Pato la Taifa mwaka 2021, huku soko la nafaka likiwa na nafasi muhimu katika kukidhi mahitaji ya ndani.
Na Fatuma Lodi.
Vijana nchini wametakiwa kutumia kilimo kama fursa ya kujiajiri na kuongeza kipato, badala ya kutegemea ajira pekee, kutokana na kuwepo kwa fursa mbalimbali katika uzalishaji wa mazao, ufugaji na biashara ya mazao.
Akizungumza kuhusu fursa hiyo, Afisa Kilimo kutoka wilayani Chemba, Maziku Ramadhan, amesema vijana wanapaswa kubadili mtazamo kuhusu kilimo na kukitazama kama shughuli inayoweza kuwa chanzo cha ajira na kipato.
Amesema baadhi ya vijana bado wanakiona kilimo kama kazi ya kawaida, hali inayochangia wengine kubaki bila ajira, licha ya sekta hiyo kuwa na fursa mbalimbali za kiuchumi.