Dodoma FM

Mbunge wa Dodoma mjini amewataka vijana kufanya kazi kwa weledi

15 September 2021, 2:12 pm

Na;Mindi Joseph.

Mbunge wa Dodoma Mjini Mh Athony mavunde amewataka vijana kufanya kazi kwa weledi pindi wanapopata nafasi ya kuaminiwa kufanya kazi Kwenye Taasisi mbalimbali Nchini.

Akizungumza na taswira ya Habari Mh Mavunde amesema vijana wanapopewa jukumu la kufanya kazi wajitume na kufanya kazi kwa weledi na maadili ili kutengeneza nafasi ya vijana wengine kuaminiwa zaidi.

Katika Hatua nyingine Mh Mavunde ameiomba serikali kuangalia sheria ya ajira no 1 ya mwaka 2015 inayoelekeza juu ya kazi zinazopaswa kufaywa na watazania na wageni ambao sio watazania kuangalia eneo hilo ili kuchochea ajira kwa vijana wengi wa kitanzania.

Aidha Vijana ni nguvu kazi ya taifa na vijana wengi wameaminiwa na kupewa nafasi kwa kuwa wana uwezo wa kufanya kazi hivyo wanajukumu la kuongeza jitihada zaidi na kuwa mfano kwa vijana wengine.