Dodoma FM

Mamlaka ya Serikali mtandao yaja na mfumo wa E. mrejesho

26 November 2021, 1:03 pm

Na; Shani Nicolous.

Mamlaka ya serikali mtandao ipo hatua za mwisho za usanifu wa mfumo unaoitwa E. mrejesho ambao utasaidia wananchi kuanadika pongezi au changamoto katika taasisi zote za umma.

Akizungumza na Dodoma fm kupitia kipindi cha Dodoma live Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi na meneja wa huduma za mamlaka ya serikali mtandao [eGA}amesema kuwa itasaidia watu kupunguza changamoto ambazo ni ngumu kuzungumzika kwa wakati hususani baadhi ya wananume wanakuwa nyuma kuripoti ukatili wanaofanyiwa na wake zao majumbani hivyo kupitia mtandao huu utarahisisha wao kutoa taarifa

Amesema kuwa wananchi waamini usalama wa huduma hizo kupitia serikali mtandao huku akizitaka taasisi za umma kujenga au kununua mifumo kutokana na viwango na muiongozo ili kuwarahisishia wananchi kutembea ofisi zote kwaajili ya huduma fulani.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wamesem kuwa seriali itambue umuhimu wa digitali katika huduma hivyo waongeze ubunifu katika huduma hizi ili kupunguza foleni na usumbufu katika ofisi mbalimbali kwaajili ya kufuata huduma.

Jamii imetakiwa kutumia mitandao hasa ya kiserili kwaajili ya kupata huduma kwa haraka na kuepusha foleni na usumbufu unaojitokeza katika ofisi mbalimbali huku serikali ikiwa hakikishia usalama na ubora wa huduma hizo.