Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuhakikisha watu wanamaliza dozi ya chanjo ya sinopharm

22 November 2021, 10:39 am

Na; Shani Nicolous.

Wito umetolewa kwa jamii kuhakikisha watu wanamaliza dozi ya chanjo ya sinopharm mara baada ya kuchanja awamu ya kwanza.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa elimu ya afya Mkoa Dr .Nassoro Ally Matuzya amesema kuwa chanjo hiyo ni lazima ichomwe mara mbili ili iweze kufanya kazi kama wataalamu wa afya walivyotoa maelekezo.

Amewapongeza wakazi wa Dodoma kwa muamko walionao katika uchanjaji kwani hali hiyo imesaidia kupunguza maambukizi kwa kiasi kikubwa na idadi ya wagonjwa waliokuwa wakitumia mashine kupua wamepungua

Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema kuwa wachache wanauelewa juu ya chanjo hii ya pili hasa katika upande wa kurudia hivyo wataalamu wa afya wasichoke kutoa elimu zaidi juu ya chanjo ya sinopharm

Sinopharm ni aina ya chanjo ambayo humlazimu mtu kuchoma kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza haitakiwi kupitisha zaidi ya siku ishirini na nane bila kurudia ya pili.