Dodoma FM

Wakazi Msisi waipongeza serikali ujenzi maabara shule ya sekondari Msisi Juu

14 June 2023, 1:50 pm

Jengo la maabara sekondari ya msisi juu. Picha na Bernad Magawa.

Maabara hizo zitachochea wanafunzi wengi wa shule hiyo ya Msisi Juu kupenda masomo ya sayansi.

Na Bernad Magawa .

Wananchi wa kata ya Msisi wilayani Bahi wameishukuru serikali kwa kujenga maabara za masomo ya sayansi kwenye shule ya sekondari Msisi Juu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwenye masomo hayo.

Akitoa shukrani hizo kwa aliyekuwa katibu tawala wa wilaya ya Bahi Jeremia Mapogo, diwani wa kata ya Msisi Mheshimiwa Mathayo Malilo amesema maabara hizo zitachochea vijana wengi kupenda masomo ya sayansi.

Sauti ya Diwani wa kata hiyo.
Picha ni jengo la shule hiyo ya Sekondari Msisi Juu iliyopo kata ya Msisi Wilayani Bahi . Picha na Bernad Magawa.

Baadhi ya walimu na viongozi wa serikali ya kijiji cha Msisi wamesema wananchi walishiriki kujenga boma ambalo serikali iliamua kulimalizia ili kuunga mkono juhudi za wananchi hao.

Sauti za walimu na viongozi.

Kwa upande wake aliyekuwa katibu tawala wa wilaya ya Bahi Jeremia Mapogo amewaagiza viongozi kuhakikisha wanautambua mchango wa wananchi wa kijiji cha Msisi ambao walijenga boma la maabara hizo kupitia nguvu kazi.

Sauti ya Jeremea Mapogo.