Dodoma FM

Wananchi wahitaji elimu zaidi juu ya wiki ya sheria

23 January 2023, 1:13 pm

Na; Mariam Matundu.

Wanachi jijini Dodoma wameshauri elimu zaidi itolewe juu ya ufahamu wa wiki ya sheria ili kutoa mwamko kwa watu wengi kutembelea katika vyombo husika  kupata msaada wa kisheria

Wamesema watu wengi hawajui nini kinaendelea katika wiki hii na hata wapi wakapate msaada hivyo wameomba kuwepo kwa utaratibu wa kuwatangazia wananchi kupitia njia mbalimbali.

Aidha wamesema watu wengi wanakutana na changamoto za kisheria hivyo wiki hii ni muhimu kwao na kusisitiza zaidi elimu ya kisheria iwafikie ipasavyo.

Hapo jana wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria Jaji mkuu wa Tanzania prof Ibrahimu Juma amesema wanaendelea kusogeza huduma za kimahakama kwa jamii kwani ndio sehemu haki inapatikana .

 Makamu wa rais wa jamhuriya muungano wa Tanzania dkt. Philp izdor mpango amesema uchumi endelevu wa wananchi utafanikiwa iwapo vyomvo vya utoaji haki vitatimiza wajibu wake katika kusikiliza na kutoa haki kwa wananchi bila upendeleo wowote.