Dodoma FM

Zifahamu shughuli za kiuchumi zinazochangia uharibifu bwawa la Hombolo

3 August 2023, 4:19 pm

Picha ni muonekano wa bwawa la Hombolo . Picha na Fahari ya Dodoma.

Serikali imekuwa ikiwasisitiza wavuvi kuwa na leseni lakini watu wengi wa eneo hili hawafuati utaratibu ili kutunza samaki wanao patikana katika bwawa hilo.

Na Yussuph Hassan.

Shughuli za kiuchumi zimekuwa zikiendeshwa kwa muda mrefu katika bwawa hili lakini shughuli za kilimo zinatajwa kuathiri bwawa kwa kiasi kikubwa kutokana na kusababisha tope kuwa jingi ndani ya bwawa hili.

Kilimo cha jembe la Trekta karibu na bwawa kinatajwa kuathiri bwawa hili kwa kiasi kikubwa kutakana na kukokota udongo unaoingia ndani ya bwawa na kusababisha tope.Picha na Fahari ya Dodoma.