Dodoma FM

Wadau na wananchi watakiwa kushiriki katika utekelezaji mpango wa Ardhi

14 July 2023, 7:33 pm

Mkuu wa wialaya ya Chamwino Mh Gift Msuya akizungumza katika mkutano huo. Picha na Seleman Kodima.

Mradi huu wa Uboreshaji usalama wa milki za ardhi unagharamiwa na Serikali kuu kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na katika Halmashauri ya Wilaya ya chamwino Mradi huo utatekelezwa katika vijiji 60 vilivyopo wilayani humo

Na Seleman Kodima.

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe Gift Msuya amewataka wadau pamoja na wananchi kushiriki vyema katika utekelezaji wa mpango wa matumizi ya ardhi kupitia mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi

Mkuu huyo wa Wilaya ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa wadau wa kujadili mpango wa matumizi ya ardhi wilaya ya chamwino  ambapo amesisitiza umuhimu wa utekelezaji wa mpango huo wa matumizi ya ardhi wilaya utasaidia kuleta matokeo chanya katika kuchochea maendeleo ya wilaya hiyo.

Sauti ya Mkuu wa wialaya ya Chamwino.
Wadau wakiwa katika Mkutano huo wilayani Chamwino. Picha na Seleman Kodima.

kwa upande wake Meneja wa Urasimishaji ardhi Vijijini kupitia mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi Bw Joseph John Osena amesema mpango huo kwa wilaya ya chamwino una lengo la kubaini aina kuu tatu za ardhi .

Sauti ya Meneja wa Urasimishaji ardhi Vijijini .